ziara ya NASA Meru

Vijana wanaopinga muungano wa NASA wamewazuia Raila Odinga na Kalonzo Musyoka dhidi ya kuhutubu katika mkutano wa hadhara uliokuwa umepangwa katika eneo fulani eneo hilo miongoni mwa mikutano kadha ya muungano huo.

Vijana hao wanaodaiwa kuimba nyimbo za kuisifu serikali ya Jubilee waliziba barabara ya kuingilia katika kituo kikuu cha magari mjini Meru hatua iliyowalazimu viongozi hao wawili kubadilisha muelekeo wa msafara wao.

Viongozi hao baadaye walipokea makaribisho kemkem mjini Meru ambapo waliwahutubia wafuasi wao kabla ya kuelekea katika eneo la Kiutune eneo bunge la Igembe ya kati ambapo waliahidi kupunguza garama ya maisha kwa siku 90 watakaoingia uongozini.

Mwisho

Total Views: 350 ,