ZIARA YA NAIBU RAIS PWANI

Naibu rais William Ruto anatarajiwa kuzuru eneo la Pwani wikendi hii.

Hapo kesho Jumamosi Ruto anatarajiwa kuongoza hafla ya kuchangisha pesa za kundi la wanawake huko Kauma, kisha baadaye ahudhurie mchango mwingine katika shule ya upili ya wasichana ya St.Johns,eneo bunge la Kaloleni,kaunti ya Kilifi.

Mbali na kuchangisha pesa,halfa hiyo pia inatarajiwa kuwa kigezo kikuu cha kubaini ni wabunge wangapi wa ODM kutoka Pwani ambao bado ni wendani wa karibu wa Ruto.

Vile vile cheche kuhusu vita dhidi ya ufisadi zinatarajiwa kutanda kwenye hafla hiyo.

Kwa upande mwingine endapo mbunge wa Malindi Aisha Jumwa atahudhuria mchango huo,atapata fursa mwafaka ya kuzidi kukiponda chama cha ODM kilichomtimua juma moja lililopita.

Picha kwa hisani

Total Views: 85 ,