Zari atangaza Kumuacha Diamond

Hatimaye mfanya biashara wa Uganda Zari Hassan ametangaza kuwa ameachana na mpenzi wake msanii wa bongo fleva  Diamond Platinumz.

Zari ametangaza uamuzi wa kuachana na Diamond kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amesema umuazi wake umechukuliwa kutokana na  tuhuma nyingi dhidi ya Diamond za kuwa na  uhusiano na wanawake wengine kila mara.

Anasema  ameamua kuulinda utu wake na kuachana naye  huku mashabiki wa Zari wakipokea habari hizo na kutoa hisia tofouti huku wengi wakimpongeza na wengine kukosoa uamuzi wake.

Diamond ni baba wa watoto wawili wa Zari ambaye ameoenakana kunyamaza kwa muda baada ya mpenziwe Diamond kukiri hadharani kudanganya katika uhusiano wao na kupata mtoto na mwanamitindo wa Tanzania Hamisa Mobetto.

Total Views: 527 ,