Yanayojiri kwenye mahakama ya upeo

Rais Uhuru Kenyatta ameimabia mahakama ya upeo kuwa marudio ya uchaguzi wa urais hayakuhitaji uteuzi mpya wa wagombea.

Kupitia kwa mawakili wake wakiongozwa na Fred Ngatia,amesema kuwa hali inayolazimu uteuzi mpya ni uchaguzi mkuu pekee na pale ofisi ya rais inapoachwa wazi kutokana na sababu zilizoratibiwa kwneye katiba.

Kwenye mawasilisho yake wakili Ngatia ameiondolea lawama tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kuwa ilikiuka sheria kwa kuendesha uchaguzi wa Oktoba 26 akisema kuwa mda wa siku 60 na uamuzi wa mahakama ya upeo haungeruhusu uteuzi mpya kufanyika.

Kadhalka ametaja hatua ya kujiondoa kwa Raila Odinga kutoka kwa kinyang’anyiro hicho kama ususiaji wa uchaguzi huku akitaja mjadala unaoendelea kuhusiana na swala hilo kama majibizano ya kuonyeshana ubabe.

Mwisho

Total Views: 221 ,