WITO KWA WAZAZI

Wito unaendelea kutolewa kwa wazazi walio na watoto waliofikisha umri wa kwenda shule kuwapeleka shule kabla hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Akizungumza na wanahabari kamishna wa kaunti ya Mombasa Evans Achoki amesema kuwa serikali imeamuru wanafunzi kwenda shule bila kulipa chochote kwa hivyo ni jukumu la mzazi kuwapeleka watoto shuleni.

Wakati huo huo Achoki amewataka machifu wote kushirikiana na wazee wa mitaa kuhakikisha kuwa watoto wote wanaenda shule huku akiahidi kutembelea kila kata na akipata watoto wakirandaranda mitaani, chifu wa eneo hilo atachukuliwa hatua za kisheria.

Total Views: 63 ,