Wezi wagonga mwamba kuiba Sanamu yenye thamani ya shilingi Milioni 340

Wahuni waliofikiri wametegua kitandawili cha kuiba sanamu katika kanisa moja huko Italia yenye thamana ya dola milioni 3.4 sawa na shilingi milioni 340  za Kenya bado wamepigwa na butwaa.

Maafisa wa polisi wanasema walibadilisha sanamu yenye thamana hiyo na bandia baada ya kupata fununu kuwa sanamu hiyo itaibiwa.

Waliibadilishwa  mwezi mmoja kabla ya wizi huo kutekelezwa na kuiweka siri.

Na sasa wezi hao wamepata mshangao kwa kufikiri kuwa wametoboa maisha.

Sanamu hiyo inathaminiwa na huwavutia watalii wengi sana.

Total Views: 50 ,