Western stima yamsajili Murungi

Huku dirisha la uhamisho katika ligi ku ya kitaifa likitazamiwa kufungwa ijumaa hii klabu ya Western stima imetwaa huduma za kijana Raymond Murugi ambae alikuwa miongoni mwa wachezaji 12 waliotemwa na wanabenki Kcb.

Kwingineko…. Wanasukari wa Sony wamekamilisha usajili wa nyota Masoud Juma kutokea klabu ya Bandari ambapo ametia sahihi mkataba wa miaka 2 na Sony.

Mkufunzi wa benchi la kiufundi katika klabu ya bandari Edward Oduor amethibitisha kuwa klabu hiyo tayari imemwachilia Masoud, ambaye anakuwa mchezaji wan ne kuondoka klabuni humo baada ya Bernard Mangoli na Edwin Wafula waliouzwa katika klabu ya Ingwee na Meshack Karani aliyejiunga na klabu ya Kakamega home boiz klwa mkopo.

Total Views: 348 ,