WAZIRI NERANDRA MODI KUJADILIANA NA RAIS

 

Waziri mkuu wa India Narendra Modi anatarajiwa kufanya mazungumzo ya kibiashara na mwenyeji wake rais Uhuru Kenyatta  katika ikulu ya Nairobi leo Jumatatu.

Waziri huyo yuko humu nchini kama sehemu ya ziara yake katika mataifa manne barani Afrika baada ya kufanya ziara nchini Tanzani,Msumbiji na Afrika Kusini.

Ziara ya Modi  hapa barani ilianza nchini Msumbiji siku ya Alhamisi ambapo alifanya mazungumzo ya kibiashara na rais wa nchini hiyo Filipe Nyusi kabla ya kusafiri kwa ndege hadi Afrika kusini kukutana na rais Jacob Zuma.

Taarifa kutoka afisi ya waziri huyo inasema amezuru bara hili akiandamana na ujumbe wa viongozi  takriban 80 wa  kibiashara.

Aidha kulingana na msemaji wa Ikulu ya rais Manoa Esipisu,ziara ya Modi itajumuisha uzinduzi wa ujenzi wa hospitali ya kutibu ugonjwa wa saratani,zaiara inayojiri siku kadhaa baada ya ile ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kukamilika Jumatano.

Total Views: 341 ,