Waziri atetea serikali dhidi ya uagizaji wa mahindi

Waziri wa kilimo Willy Bett ametetea hatua ya serikali ya kuagiza mahindi akisema uhaba wa bidhaa hiyo hapa nchini ulisababishwa na hatua ya kufichwa kwa bidhaa hiyo kwa lengo la kuongeza bei almaarufu kuhodhi.

Akiongea alipofika mbele ya kamati ya bunge kuhusu kilimo kuangazia uagizaji huo tata wa mahindi ,waziri alisema kulikuwa na mavuno duni msimu uliopita,hatua alisema ilisababisha baadhi ya wakulima kuhodhi  mahindi wakitarajia bei kuongezeka.

Alisema hata baada ya serikali kuongeza bei ya gunia ya kilo 90  ya mahindi hadi shilling elfu-tatu,baadhi ya wakulima waliendelea kuhodhi bidhaa hiyo,hatua alisema iliwalazimisha wasagaji nafaka kuongeza bei.

Mwisho

Total Views: 296 ,