Wazira ya Leba yawarai Wauguzi Kusitisha Mgomo

Waziri wa leba Ukur Yattani ameutaka muungano wa wauguzi KNUN kusitisha mgomo wa wauguzi unaoendelea kuambatana na agizo la mahakama  kama ishara ya nia njema dhidi ya majadiliano yanayoendelea.

Hatua hiyo kulingana na waziri itatoa  mazingira mwafaka kwa mchakato wa upatanisho.

Kufikia sasa waziri Yattani anasema mchakato huo unaendelea huku masuala mengi yakiwa tayari yameafikiwa.

Huku haya yakijiri, wauguzi katika kaunti ya Kisii wana hadi kesho kujibu barua ya kwa nini wasichukuliwe hatua kufuatia mgomo huo.

 

 

Total Views: 78 ,