Wazee waonywa dhidi ya kufukuza wake zao Kwa kukosa Kupata Watoto

Baraza la wazee kaunti ya kwale limetoa Changamoto kwa jamii   kukomesha tabia ya kuwafukuza wake zao pindi wanapochelewa ama kushindwa kupata watoto katika ndoa.

Wazee hao  wanaodai kuwa imekuwa tabia  ya vijana kwale kuhusisha tatizo la ukosefu wa uzazi na ushirikina au laana  katika ndoa  ambapo wanawake  hulaumiwa, kukejeliwa na  hata kutendewa unyama na waume zao .

Vile vile wazee hao wametaka wenyeji kupuzilia mbali dhana potovu na badala yake kuwataka wanaokosa watoto katika ndoa kutafuta matibabu na ushauri nasaha kwa wataalamu badala ya kuvunja ndoa pale panapokosekana watoto.

Total Views: 110 ,