Wazee wa Kaya waunga mkono wabunge waasi wa CORD

Viongozi  wakisiasa walioasi mrengo wa upinzani CORD kutoka hapa Pwani pamoja na wazee wakaya wamezindua kampeni ya kugeuza eneo hili kutoka ngome ya upinzani hadi Jubilee.

Wakiongea katika  hoteli moja  hapa Mombasa,viongozi hao waliounda azimio kwa jina “Serena Declaration”walisema watafanya msururu wa mikutano ya hadhara katika kaunti zote sita za eneo la pwani  kuanzia wiki ya kwanza ya mwezi Agosti kuwaelimisha wananchi kwa lengo la kuwaregesha serikalini.

Viongozi hao sita marafiki wa karibu wa mbunge wa Kilifi Kaskazini Gedeon Mung’aro ni pamoja na  Khatib Mwashetani wa  Lunga Lunga , mwakilishi wa kike wa kaunti ya Kwale Zainab Chidzuga, Mustafa Idd  wa Kilifi kusini,  Shariff Athman  wa Lamu mashariki na Peter Shehe wa  Ganze.

Kwa upande wake mbunge Gedion Mung’aro amemuonya aliyekuwa katibu Mkuu wa chama cha Cord Ababu Namwamba asibadili msimamo wake wa kujihuzulu kama katibu wa chama hicho akiongeza kuwa Cord imekosa mwelekeo.

Total Views: 598 ,