Wazee wa kalenjin wamtaka,naibu rais kudhibiti usukuani wa URP

RUTOBaadhi ya wazee wa jamii ya Wakalenji wamemtaka naibu wa rais William Ruto kuweka mikakati ya dharura ya kushinikiza uwiano na viongozi waasi wa chama cha URP kwa umoja wa kisiasa miongoni mwa jamii hiyo.

Wakiongozwa na Simeon Murkelda na William Sawe,wazee hao wametoa wito kwa naibu huyo rais kuharakisha hatua ya kufanyika kwa mkutano wa upatanisho kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2017 ili kuepuka mgawanyiko.

Wamemtaka Ruto kutopuuza lalama za viongozi hao wanaodaiwa kuwa waasi wa chama cha URP ikizingatiwa kuwa hatua hiyo inatishia kusababisha mgawanyiko kwa msingi wa kijamii na kisiasa kati ya eneo la South Rift na North Rift.

Miongoni mwa viongozi hao ni Gavana wa Bomet Isaac Ruto,Wabunge Oscar Sudi wa Kapseret,Alfred Keter wa Nandi hills na Johana Ng’eno wa Emurua Dikir waliodhihirisha uasi wao kwa kumpigia debe mgombea wa KANU katika uchaguzi mdogo wa Useneta wa Kericho.

Mwisho

Total Views: 388 ,