WAVUVI KILIFI

Wavuvi katika kaunti ya Kilifi wameonywa dhidhi ya matumizi ya vifaa vya uvuvi vinavyoharibu mazingira ya baharini.

Akiongea katika zoezi la kusafisha ufuo wa bahari mjini Kilifi, afisa mkuu wa mazingira katika gatuzi la Kilifi Maryam Jenneby amesema kuwa wizara yake itashirikiana na wizara ya uvuvi katika kaunti hiyo pamoja na ile ya kitaifa kupitisha sheria inayopania kuchukulia hatua wavuvi wanaotumia vifaa vinavyoharibu mazingira ya bahari.

Aidha maoni hayo yameungwa mkono na mkurugenzi wa mazingira katika kaunti ya kilifi Bi. Zena Hasssan, ambapo amesema kuwa ni sharti viwanda vyote vinavyotoa maji taka baharini vitimize sheria ili kuzuia uchafuzi wa maji baharini.

 

Total Views: 15 ,