Wauguzi Mombasa wamtaka Gavana Joho kusitisha kampeini ili kutatua mgomo unaoendelea

Katibu mkuu wa muungano wa wauguzi tawi la Mombasa Peter Maroko amemtaka gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho kusitisha kampeni za kisiasa na badala yake aungane na magavana wengine kujadiliana jinsi ya kumaliza mgomo wa wauguzi.

Akizungumza na pwani Fm kwa njia ya simu Maroko amesema kuwa ni wakati mwafaka ambao serikali ya kaunti inafaa kujitokeza na kushiriki majadiliano kati ya washikadau husika ikiwemo viongozi wa wauguzi na baraza la magavana.

Kadhalika ameishtumu tume ya kuwianisha mishahara SRC kwa kuwaorodhodhesha katika kiwango cha chini katika mipangilio yao huku akisema kuwa hatua ya baraza la magavana kuwaajiri wauguzi hakutaleta suluhu yoyote katika sekta ya afya.

Mwisho

Total Views: 225 ,