Watumishi wa Umma Kuhesabiwa

Wizara ya fedha   inatarajiwa kuanza shughuli ya  kuhesabu watumishi wa umma waliostaafu juma  lijalo ili kuondoa  wafanyakazi waliosataafu  bandia  wanaochangia kupotea kwa mamilioni ya  fedha za malipo ya uzeeni kila mwezi.  

Shughuli hiyo itahusisha  wafanyakazi  laki tatu wa umma waliostaafu kufika kwenye vituo vya Huduma  kote nchini. 

Shughuli hiyo inalenga kupunguza mzigo ya malipo kwa wafanyakazi wa umma waliostaafu ambayo yanatarajiwa kuzidi shilingi  bilioni 100 mwaka ujao.

Kwenye tangazo lililochapishwa katika magazeti ya humu nchini shughuli hiyo itaanza tarehe 11  mwezi february  na kukamilika tarehe  3 mwezi may  mwaka huu.W

Total Views: 332 ,