watu zaidi ya milioni mbili waendelea kukabiliwa na ukame

Zaidi ya wakenya milioni 2 kutoka maeneo kame na kame kiasi wameendelea kutaabika na makali ya ukame yaliyopelekea vifo vya mifugo na watoto kuacha masomo.

Nane kati ya kaunti 23 zinazokumbwa na ukame huo zitapokea msaada wa chakula kinachogharimu shilingi milioni 16 kutoka kwa ubalozi wa china humu nchini, kama njia moja wapo ya kukabiliana na madhara ya ukame huo.

Vyakula hivyo vinajumuisha tani 48 za unga wa mahindi,tani 48 za unga wa ngano pamoja na mafuta ya kupikia na vitagawanywa katika kaunti za Turkana, Samburu, Marsabit, Lamu, Laikipia, Baringo, Isiolo na  Kitui.

Akizungumza wakati wa kupokea misaada hiyo katibu wizara ya mipango maalum Josepheta Mukobe amesema serikali kwa ushirikiana na wadau mbali mbali wanaendelea na mipango ya kuwafikia wakenya wanaohitaji misaada kwa dharura.

Total Views: 304 ,