Watatezi wa Gavana Joho Wazungumza

Wabunge wawili wendani wa gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho wamewakashifu wenzao wanaotaka  naibu rais William Ruto kupata uungwaji  mkono na  eneo hili la Pwani wakidai wanahujumu umoja na maendeleo.

Mbunge wa Ganze Teddy Mwambire  na Omar Mwinyi wamewataja wenzao kama wasaliti na wanaotaka umaarufu.

Mwinyi alisema wabunge hao wanaomuunga mkono naibu rais wanafaa kupigania ili watu zaidi wapate ajira katika Bandari na mamlaka ya uchukuzi wa baharini humu nchini.

Kwa upande wake Mwambire aliye pia mwenyekiti mdogo wa chama cha ODM katika kaunti ya Kilifi hajawahi kuhudhuria mikutano ya Ruto hapa Pwani akisema haelewi inalenga kuafikia nini.

Wabunge waliotangaza hadharani kuunga mkono azma ya naibu huyo wa rais ya kuwania urais mwaka 2022 ni pamoja na Aisha Jumwa wa Malindi,Suleiman Dori wa Msambweni,Badi Twalib wa Jomvu miongoni mwa wabunge wengine.

Total Views: 97 ,