Wasiwasi Kilifi Kutokana na Idadi ya Wanaojiunga Kidato cha Kwanza

Wadau wa elimu kaunti ya Kilifi wameelezea wasiwasi wao kuhusiana na idadi kubwa ya wanafunzi wanaojiunga kidato cha kwanza eneo hilo.

Katibu wa chama cha KNUT tawi la Malindi Fred Nguma amelalamikia hatua hiyo akisema shule nyingi eneo hilo hazina vifaa vya kutosha vya kusomea jambo ambalo limesababisha msongamano katika madarasa hatua anayoitaja kuhujumu ubora wa elimu.

Siku chache zilizopita waziri wa elimu Amina Mohammed alitoa tangazo kwamba zaidi ya asilimia 70 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la nane KCPE mwaka jana tayari wamejiunga na shule za upili.

Total Views: 91 ,