washukiwa watatu wakamatwa na shehena ya pembe za ndovu

Maafisa wa upelelezi wamefanikiwa kukamata shehena ya pembe za ndovu yenye thamani ya shilingi milioni 12 katika eneo la Mariakani kaunti ya Kilifi.

Kikosi cha maafisa hao kutoka idara ya upelelezi wa jinai DCI na wa huduma ya kuhifadhi wanyamapori waliokuwa wakifuatilia  ripoti za kijasusi walifanikiwa kuwatia nguvuni washukiwa watatu na shehena hiyo ilikiwa  imefichwa ndani ya nyumba.

Mkuu wa polisi katika eneo hilo Ramson Lolmodoni amesema washukiwa hao wanaaminika kuwa na uhusianao na walanguzi wa pembe za ndovu mashinani.

Total Views: 281 ,