Wasafari Washangazwa na Abiria Mwenzao aliyetoa Nguo

Wasafiri katika uwanja wa ndege huko Moscow nchini Urusi walijionea vitimbi vya bure pale msafiri mwenzao alipotoa nguo zote na kubakia uchi wa mnyama kwa kile anachodai kuwa hali hiyo ingemsaidia kuwa na wepesi wa kupaa maarufu kama aerodynamic.
 
Kanda ya video inaonyesha jamaa huyo mwenye umri wa miaka 38 akiwa amesubiri kuabiri ndege ya kampuni ya Ural na kisha baadaye kukimbia kuingia kwenye ndege hiyo alipogundua wahudumu wa ndege walikuwa wakimfuata ili kumuzuia.
 
Basi alianza kupiga mayowe huku akisema kuwa yeye hupaa kwenye ndege na uhuru zaidi ikiwa uchi wa mnyama.
 
Picha kwa wahisani

Total Views: 49 ,