Wanawake Tuchape kazi,Asema Waziri, Amina Mohammed

CS AMINA MOHAMMEDWaziri wa maswala ya kigeni Bi Amina Mohammed ametoa wito kwa viongozi wanawake nchini kujibidisha zaidi katika utekelezaji wa majukumu yao dhidi ya wenzao wanaume ikitiliwa maanani uwezo walio nao.

Akizungumza katika kongamano kuhusu uongozi wa akina na mama hapa Mombasa Bi Amina amesema kuwa ni kupitia juhudi na ubora wa utendakazi wa wale walio uongozini ambapo wanawake nchini wataweza kupata nyadhfa zaidi serekalini na pia sekta ya kibinafsi.

Aidha ametoa wito wa kujitokeza kwa wanawake zaidi kwenye nyadhfa kuu za kazi zinazotangazwa ikitiliwa maanani utafiti wa hivi punde uliobaini kuwa ni asilimia 30 tu ya wanawake wanaojitokeza dhidi ya asilimia 70 ya wanaume katika mahojiano ya kikazi.

Kadhalka mwenyekiti wa tume ya uainishaji wa mishara nchini SRC Bi Sarah Serem amewataka wakina mama wanaofanikiwa kupata nyadhfa husika kuwa tayari kwa makabiliano dhidi ya changamoto husika kwa manufaa ya utendakazi wao.

Mwisho

Total Views: 381 ,