“WANAWAKE HAWATA KANDAMIZWA” AAHIDI MISHI MBOKO

Mbunge wa Likoni Mishi Mboko ameahidi kushinikiza uundaji wa sheria zitakazohakikisha kuwa wanawake humu nchini hawakandamizwi.

Akipokea malalamishi kutoka kwa wanawake kaunti ya Mombasa,Mishi anasema atawarai wabunge wenzake kuhakikisha kuwa sheria zinazowanyanyasa wanawake zinafanyiwa ukarabati.

Wakati huo huo mbunge huyo amelalamikia kukithiri kwa dhuluma dhidi ya wanawake.

Kutokana na hilo,Mishi anapendekeza unyanyasaji dhidi ya wanawake kutangazwa kuwa janga la kitaifa.

Mbunge huyo amesema hayo alipoungana na wanawake mjini Mombasa wakati wa maandamano kuadhimisha siku ya wanawake duniani.

Picha kwa hisani.

Total Views: 76 ,