Wana Mazingira na marufuku ya mifuko ya plastiki

Wana mazingira wameunga mkono marufuku dhidi ya matumizi ya mifuko ya plastiki nchini na kuahidi kupeana msaada wao wa kitaalam kuhakikisha kuwa marufuku hiyo inafualu kwa manufaa ya taifa hili.

Kwenye taarifa, vuguvugu la Green Belt na Greenpeace Afrika, yameunga mkono hatua hiyo ya serikali wanaoitaja kuwa ya kijisiri na iliyosubiriwa kwa mda mrefu baada ya nchi nyengine ikiwemo Rwanda kutekeleza marufuku hiyo mapema.

Mkurugenzi mkuu wa Green Afrika ,Njeri Kabeberi amesema hatua hiyo inadhihirisha kuwa nchi ya Kenya imekomaa katika maswala ya mazingira huku mwenyekiti wa bodi ya vugu vugu la Green Belt Marion Kamau akisema athari za mazingiri zitapungua pakubwa.

Mwisho

Total Views: 216 ,