Waliokamatwa kwa maandamano ya CORD Mombasa Waachiliwa

Spika wa bunge la kuanti ya Mombasa Thaddeus Rajuwai na muwakilishi wa wadi ya Junda Oswago Honje waliachiliwa huru baada ya kukamatwa wakati wa maandamano ya Cord hapa Mombasa.

Awali Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho walikuwa kwenye kikao cha faragha na kamanda wa polisi hapa Mombasa Francis Wanjohi ambapo inadaiwa walikuwa wakizungumzi kuhusu kuachiliwa kwa wawili hao.

Viongozi wa CORD hapa mombasa wakiongozwa na Gavana Ali Hasan Joho,wabunge Abdhulswamad Nassir,Rashid Bedzimba,Badi Twalib,muwakilishi wa kike katika kaunti ya Mombasa Mishi Mboko na wawakilishi wa wadi waliwasilisha lalama zao kwa IEBC.

Mjini Kilifi kulikuweko na ulinzi mkali wa maafisa wa usalama katika ofisi za IEBC licha ya kutokuweko kwa maandamano kama ilivyodhaniwa awali.

Haya yanajiri huku mkurugenzi wa mawasiliano katika chama cha ODM Phili Etale akisisitiza kuwa maandamano hayo ni halali na yako kwa mujibu wa katiba.

Mwisho

Total Views: 454 ,