wakufunzi zaidi watuma maombi kunoa Shujaa 7s

Jumla ya wakufunzi watano kutoka humu nchini katika mchezo wa raga wametuma maombi ya kuchukuwa wadhfa wa mkufunzi mkuu katika timu ya taifa ya raga ya wachezaji 7 upande.

Taarifa zinasema kuwa Paul Murunga ambaye alimsaidia Benjamin Ayimba kufika awamu ya Main cup mwaka 2016 ni mmoja wa waliotuma maombi huku shirikisho la mchezo huo likithibitisha kuwa wakufunzi wa kigeni 7 pia wametuma maombi kwa nafasi hiyo inayomilikiwa na Innocent ‘’Namco’’ simiyu..

Mkataba wa Simiyu unakamilika mweji ujao wa oktoba na aliweka bayana kuwa hatotaka mkataba zaidi baada ya kuongoza shujaa kwa misimu miwili.

Total Views: 162 ,