Wakenya Kuadhimisha siku ya Mashujaa

Rais Uhuru Kenyatta ataongoza wakenya kuadhimisha siku kuu ya Mashujaa hii leo katika uwanja wa Bukhungu katika kaunti ya Kakamega.

Inabashiriwa kuwa huenda siasa za kilimo cha mahindi na miwa zikatawala maadhimisho hayo kutokana na wakulima wa mazao hayo kuathirika na mapato.

Hatibu wa ikulu Kanze Dena asema kuwa rais Kenyattta anapendekeza kubuniwa kwa mpango wa kufufua viwanda vya miwa badala ya kuendelea kuhofia hazina kutumika vibaya.

Wanaotarajiwa kuhudhuria maadhimisho hayo ni rais wa Namibia Hage Geingob ambaye ndiye mgeni mashuhuri.

Total Views: 199 ,