Wakaazi wa Malindi wanaopakana na uwanja wa ndege kufidiwa mwezi wa nne

Mwenyekiti wa tume ya kitaifa kuhusu ardhi Dkt Mohammed Swazuri amewahakikishia wakaazi wa Malindi watakaolazimika kuhama ili kupeana nafasi ya upanuzi wa uwanja wa ndege wa Malindi kuwa watapata fidia zao katika kipindi cha mwezi mmoja ujao.

Akizungumza katika eneo la Kwachocha mjini Malindi,Swazuri amewataka wakaazi hao kutohofu kwani tume yake itahakikisha kuwa kila muathiriwa wa upanuzi huo analipwa fidia inayostahili kwa mujibu wa rasilimali iliyo katika ardhi yake.

Mwisho

Total Views: 614 ,