Wajasiriamali Hawataki Kufanyike Uchaguzi Malindi

Wawekezaji na wakaazi mjini Malindi wameapa kuuzima mdahalo kuhusu uwezekano wa kufanyika kwa uchaguzi mdogo katika eneo bunge hilo,wakisema kuwa hatua hiyo itaathiri uchumi.

Wakiongozwa na mkurugenzi wa chama cha wafanyibiashara na wenye viwanda eneo hilo Fuad Kombe,wajasiriamali hao wanawalaumu vinara wa ODM hasa katibu mkuu Edwin Sifuna,

kwa kile wanachodai kama kushinikiza uchaguzi huo utakaoathiri biashara zao.

Kulingana na Kombe,chaguzi zimekuwa zikiathiri pakubwa biashara katika mji huo wa kitalii.

Wafanyibiashara hao sasa wanamtaka kinara wa ODM Raila Odinga kujadiliana na gavana Amason Kingi ili kutatua utata ulioko eneo hilo.

Total Views: 86 ,