Waislamu nchini washerehekea siku kuu ya Eid-ul fitr

Waislamu nchini wameungana na wenzao ulimwenguni kuadhimisha siku kuu ya Eid-ul fitr huku kukiwa na wito umoja miongoni mwa wakenya wakati nchi hii inapoelekea uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2017.

Akizungumza hapa mombasa baada ya swala la Eid katika uwanja wa shule ya msingi ya Ronald Ngala aliyekuwa kadhi mkuu Sheikh Hamad Kassim ametoa wito wa amani ulimwenguni kwa kuepuka chuki.

Na jijini Nairobi , viongozi wa kiislamu wakiongozwa na Imam wa mskiti wa Jamia Sheikh Mohamed Swaleh na kiongozi wa wengi katika bunge la taifa Adan Duale wameonya dhidi ya kuwagawanya wakenya kwa msingi wa kisiasa na kidini.

Mwisho

Total Views: 498 ,