wahudumu wa boda boda watakiwa kujisajili Changamwe

 

Waendesha bodaboda wote katika eneo bunge la Changamwe wametakiwa kujisajili  katika maeneo wanakofanyia kazi kwenye harakati za kukabiliana na visa vya uhalifu eneo hilo.

Akizungumza na wanahabari afisini mwake naibu kamishna wa kaunti katika kaunti ndogo ya Changamwe Benjamin Njoroge,amesema kuwa tayari amekuwa na vikao na wahudumu hao wa bodaboda ili kuhakikisha biashara hiyo inaendelea kuwahudumia wananchi.

Amesema  katika eneo hilo kuna vituo 46 vya boda boda ambavyo viko chini ya wenyekiti na kuwataka kila anayejiunga na sekta hiyo kuwa na stakabadhi husika  sawia na kufuata sheria vilivyo.

Wakati huo huo mbunge wa eneo hilo Omar Mwinyi Shimbwa amesema kuwa vijana wanaohudumu kama  waendesha boda boda hupitia changamoto nyingi za kiusalama hivyo  ni lazima kuwe na utaratibu wanapobeba abiria.

 

Total Views: 385 ,