Wafuasi wa NASA wakaidi agizo la serikali na kuandamana,huku baadhi wakijeruhiwa

Mamia ya waandamaji wa muungano wa NASA wamemiminika katika barabara za miji mikuu nchini licha ya serikali kupiga marufuku maandamano bila ya idhini kutoka kwa idara ya polisi.

Watu wawili wameuwawa  kwa kupigwa risasi eneo la Bondo huku wengine wawili wakijeruhiwa wakati polisi walipofyatua risasi dhidi ya kundi la waandamanaji walikua wakirusha mawe kwa kituo cha polisi huku mwengine akipigiwa risasi kichwani Kisumu.

Hapa Mombasa Polisi waliwarushia vitoa machozi waandamanaji waliokuwa wakijaribu kuingia kati kati mwa jiji huku polisi wa kukabiliana na gasia wakishika doria mapema jijini Nairobi ili kuzuia maandamo.

Katika maeneo ya magharibi mwa Kenya na vile vile Kisumu yanayoaminika kuwa miongoni mwa ngome za kinara wa Upinzani Raila Odinga,waandamanji walifunga baadhi ya barabara muhimu na kuchoma magurudumu.

Kaimu waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang’i alipiga marufuku maandamano katika miji mikuu ikiwemo Nairobi,Kisumu na hapa Mombasa huku viongozi wa upinzani wakisisitiza kukaidi agizo hilo na kuendelea na maandamano kila siku ya juma.

Mwisho

Total Views: 161 ,