Wafanyakazi Walipwa Matofali

Si jambo la kawaida wafanyakazi wanaogoma kupewa kile wanachofanyia kazi badala ya mishahara wanaodai.

Lakini hayo yamefanyika nchini Uchina ambapo wafanyakazi wa  kiwanda cha matofali kusini mashariki mwa Uchina  inaropotiwa wamepewa matofali badala ya mshahara.

Wafanyakazi hao wanadaiwa kudai  mishahara yao yenye thamani ya $14,050, sawa na takriban  shilingi Milioni 1.6 za Kenya.

Kwa mujibu wa shirika la habari Xinhua, takriban wafanyakazi 30 wa kiwanda hicho huko Nanchang, katika jimbo la Jiangxi , walikubali kulipwa matofali 290,000 badala ya mshahara wanaodai.

 

Total Views: 267 ,