Wafanyabiashara Kongowea Waandamana kwa Madai ya Kuhangaishwa

Wafanyabiashara wa viazi katika soko la Kongowea hapa Mombasa wameandamana hadi katika afisi za kaunti ya Mombasa  kwa kile wanachokitaja kuwa kuhangaishwa na askari wa kaunti ya Mombasa kwa wiki moja sasa.

Wafanyabiasahara hao  wanapinga kulazimishwa kuuzia viazi vyao katika orofa ya tano ya jumba jipya sokoni humo jambo wanalopinga vikali.

Kadhalika wameitaka serikali ya kaunti kuingilia kati na kuwaruhusu kuuzia bidhaa zao mahali pao pa kawaida au maeneo ya chini ya jumba hilo jipya ili waweze kuwafikia wateja wao u.

Total Views: 150 ,