Waenezaji chuki kwa WhatsApp kukabiliwa

Hatibu wa idara ya polisi nchini Charles Owino amesema kuwa wasimamizi wa makundi mbali mbali ya mtandao wa WhatsApp watafunguliwa mashtaka iwapo makundi yao yatasambaza jumbe za chuki.

Kulingana na hatibu huyo, polisi hawataruhusu mtu yeyote kutatiza amani wakati huu wa uchaguzi ikitiliwa maanani umuhimu wake kwa taifa hili kwenye harakati ya kuepuka uwezekano wowote wa kushuhudiwa kwa vurugu.

Haya yanajiri huku wataalam wa sheria kuhusu mtandao wakiibua maswali kuhusu sheria itakayotumika kuwafungulia mashtaka wasimamizi wa makundi hayo ya mtandao wa WhatsApp ikizingatiwa kuwa hawana uwezo wa kuzuia jumbe moja kwa moja.

Mwisho

Total Views: 328 ,