Wacheza Densi Tupu Uchina

Waandalizi wa mazishi nchini Uchina  hasa sehemu za vijijini huwalipa wacheza densi tupu kuwatumbuiza waombolezaji kwenye mazishi.

Duru zinaarifu  kuwa wacheza utupu hutumiwa kuwavutia watu wnaaohudhuria mazishi kwa sababu uwepo wa watu wengi kwenye mazishi huonekana kama heshima kwa marehemu.

Waandali hao hasa sehemu za mashambani hutumia  pesa nyingi hata kuliko mapato yao , kuwalipa wuigizaji, waimbaji, wachekeshaji na wacheza utupu kuwatumbuiza wale waliofiwa.

Hata hivyo serikali ya Uchina inajaribu kudhibiti hali hiyo na kuwatia nguvuni wanaofanya hivyo.

Total Views: 252 ,