Waathiriwa wa Mafuriko Kilifi wahamishiwa maeneo salama

Takriban familia elfu sita zimeokolewa kutokana na mafuriko katika kaunti ndogo ya Magarini na Malindi baada ya jeshi la kenya la Angani kuingilia kati na kutumia ndege maalum kwa shughuli hiyo.

Kulingana na mmoja wa waathiriwa Bi Josphine Unda walifanikiwa kufikia maeneo salama baada ya juhudi hizo huku wakitoa wito kwa wahisani kujitokeza na msaada baada ya kushindwa kuokoa chochote.

Afisa wa shirika la Action Aid Cosmas Meng’anyi amesema kuwa waathiriwa wote kutoka kwa takriban vijiji 50 vilivyoathirika wamehamishiwa maeneo salama huku wengine wanaoishi maeneo ya chini wakitakiwa kuhama kabla ya kusombwa na maji hayo.

Mama unda ni mmoja wa waathiriwa.

Mafuriko hayo yanajiri baada ya mto sabaki kuvunja kingo zake kufuatia mvua kubwa inayoendelea kushuhudiwa katika maeneo mbali mbali ya nchi.

Mwisho

Total Views: 309 ,