Waakazi wa Mkwakwani Wataka Kufidiwa

Wakaazi wa kijiji cha Mkwakwani liliko eneo la ukunda  kaunti ya kwale wanaitaka serikali kuwafidia  shilingi milioni 400   kwa kipande cha ardhi chenye zaidi ya ekari 100  walichokitoa kwa ujenzi wa  kiwanja kidogo cha ndege cha Mkwakwani

Nyangasi Mohamed anataka pia familia 300 kuhamishwa kwa sababu wamechoka kusikia kelele za ndeg zinatua na kupaa huku akisema kuwa ameshangazwa na hatua ya serikali kudinda kuwafidia ili waweze kuondoka mahali hapo.

Sasa wakaazi hao wanakumbwa na hali ya swintofahamu baada ya mwenyekiti wa tume ya  ardhi Mohamed Swazuri kunukuliwa akisema   mwaka jana kwamba wakaazi hao hawatafidiwa.

Total Views: 156 ,