WAACHENI WASOME

Mbunge wa Matuga  kaunti  ya  Kwale  Kassim  Sawa Tandaza  amewataka wakuu wa shule za upili  katika eneo hilo la Matuga  kutowarudisha nyumbani wanafunzi  hususan wakidato cha nne kwa kisingizio cha karo .

Tandaza aliyekuwa akizungumza  katika shule ya upili ya  wasichana  ya  Rose Mwakwere   huko Matuga  amesema kuwa wanafunzi kukosa  kuhudhuria masomo  kikamilifu  pia  inachangia  matokeo duni katika mitihani wa kitaifa .

Amedokeza kuwa japo serikali  inasaidia kulipa karo nusu kwa wanafunzi  bado baadhi ya wazazi hawana uwezo wa kulipia  karo  inayosalia   akiahidi  kuwasaidia wanafunzi  hao ili kuona kuwa wanapata elimu bora.

Total Views: 57 ,