VYAKWELI ATUTUZWA KIMATAIFA KUTOKANA NA JITIHADA KATIKA SEKTA YA MAJI

Afisaa mkuu wa mawasiliano katika kampuni ya huduma za maji na maji taka ya Nairobi,Mbaruku Vyakweli amekabidhiwa taji la kuwa miongoni mwa watu 51 wenye ushawishi mkubwa katika sekta ya maji duniani mwaka 2019.

Kongamano hilo huandaliwa kila mwaka kuwatambua viongozi ambao mchangao wao umeyageuza maisha ya wengine.

Vyakweli ambaye asili yake ni eneo la Likoni kaunti ya Mombasa,alikabidhiwa taji hilo nchini India mapema wiki hii,kwenye kongamano la viongozi wa sekta ya maji duniani.

Mbali na taji hilo Vyakweli amewahi kuhudumu kama makamu wa rais kitengo cha sayansi na maswala ya baraza la kiufundi la muungano wa maji barani Afrika kuanzia mwezi Machi 2016 hadi Februari 2018.

Kabla ya hapo aliwahi kuchaguliwa katika kamati kuu ya kimataifa ya umoja wa mataifa (UNHABITAT) ya wahudumu katika sekya maji duniani (GWOPA) kwa miaka sita.

Mnamo mwaka 2017 Novemba alichaguliwa tena kama naibu gavana katika bodi ya magavana ya baraza la maji duniani kwa muda wa miaka mitatu.

 

 

 

 

 

 

Total Views: 83 ,