VURUMAI YA BODA BODA MALINDI

Hali ya mshike mshike ilishudiwa baada ya wadudumu wa boda boda mjini Malindi kwa ushirikianao na wale wa Watamu kutishia kuchoma maiti iliyokuwa imewekwa ndani ya jeneza.

Inaarifiwa kuwa wahudumu  hao waliokuwa wamejawa na gadhabu walitishia kulipiza kisasi kwa kuuchoma mwili wa marehemu kwa kile walichodai kuwa  kabla ya kifo chake, marehemu alikuwa akishirikiana na wahuni kuiba pikipiki.

Ni hali iliyowalazimu maafisa wa polisi zaidi ya 12 waliokuwa wamejihami kuingilia kati kutuliza vurumai hilo huku wakilazimika kushika doria kwenye mazishi ya mwanamke huyo katika kijiji cha Kajajini.

Katika hali hiyo  waombolezaji waliokuwa wamefika katika eneo hilo hawakupewa fursa ya kuutazama mwili kwani ulipelekwa moja kwa moja hadi kaburini.

Marehemu Kanze Mathole mwenye umri wa miaka 30, alijiuwa kwa kujitia kitanzi tarehe 27 Januari mwaka huu, katika eneo la Marereni kaunti ndogo ya Magarini.

Total Views: 105 ,