VIONGOZI MOMBASA WAUNGA MKONO

Viongozi kutoka kaunti ya Mombasa kwa sauti moja wameutaja mkutano kati ya rais  Uhuru Kenyatta na kiongozi wa muungano wa CORD Raila Odinga  hapo jana kama njia mojawapo ya kuonyesha umoja na uwiano wa kitaifa.

Wakiongozwa na gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho kwenye sherehe za madaraka zilizofanyika katika uwanja wa Tononoka hapa Mombasa viongozi hao wamesema kuwa wana imani kwamba mkutano huo utazaa matunda hasa kuhusu suala la  kuwashinikiza makamishina wa IEBC kuondoka afisini.

Kuhusu swala la usalama  kamishina wa kaunti hii ya Mombasa Maalim Mohammed amesema kuwa anapanga kukutana na viongozi wa eneo hili kuweka  mikakati ya kudumisha usalama aliotaja  kukumbwa na changamoto miongoni mwa wananchi.

Kadhalika Mohammed amewataka wananchi kushirikiana na maafisa wa polisi kwa kutoa taarifa zozote za kihalifu wanazoshudia.

Total Views: 306 ,