Viongozi mjini Lamu kuenda mahakamani kupinga ujenzi wa bandari.

Viongozi katika kaunti ya Lamu wametishia kuelekea mahakamani kuwasilisha kesi ya kupinga hatua ya tume ya ardhi nchini kutenga zaidi ya ekari elfu ishirini kwa mradi wa ujenzi wa bandari ya Lamu LAPSSET.

Gavana wa kaunti hiyo Isaa Timammy amesema hatua ya NLC kutenga ekari elfu 28 za ardhi kwa ujenzi wa bandari hiyo ni kinyume cha katiba na kwamba wataelekea mahakamani kuzuiya hatua hiyo.

Akiongea katika eneo la Witu wakati wa kukagua miradi mbalimbali ya kaunti,Timammy amesema ameshangaa kusikia kwa tume ya ardhi imeamua kutenga kiasi hicho cha ardhi bila kufanya mashauriano.

Timammy ambaye alikuwa ameandamana na naibu wake Erick Mugo amesema hawatakaa wakitazama ardhi ya umma ikitumiwa na taasisi za serikali bila idhini yao na kwamba watataufuta utatuzi kamili wa suala hilo.

Hata hivyo amesema serikali yake haipingi mradi huo wa ujenzi wa bandari LAPSSET lakini hawatajilazimisha kuunga mkono mradi ambao utaponyoka na ardhi ya wakaazi.

Total Views: 463 ,