Vinara wenza wa NASA wataka mazungumzo kuhusisha wakenya wote

Vinara wa Nasa waliotofautiana na hatua ya Raila Odinga kutia saini mkataba na rais Uhuru kuanzisha mchakato wa kuleta maridhiano nchini wamedumisha kuwa wanaunga mkono mdahalo lakini wakasisitiza kuwa mdahalo huo unafaa kuhusisha wakenya wote.

Kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi aliyesoma taarifa fupi kwa niaba ya vigogo wanne wa NASA amesema mazungumzo yanafaa kuandaliwa kwa misingi ya maswala ambayo wamekuwa wakitetea.

Maswala hayo ni pamoja na haki katika uchaguzi, ugatuzi, ukabilianaji wa umaskini , utovu wa usalama na kulinda idara ya mahakama.

Akiongea baada ya mkutano wao huko Athi River amesema mkutano huo ulinuiwa kumpa Raila Odinga nafasi ya kuwapasha habari kuhusu mashauriano yao na rais Uhuru Kenyatta siku ya Ijumaa jambo ambalo Mudavadi amesema Raila alifanya kwa njia ya kuridhisha.

Alisema habari kuhusu yale yaliyoafikiwa kwenye mkutano huo yatawasilishwa kwa vyama husika ambapo mkutano mwingine utaandaliwa na  mwelekeo utakaochukuliwa kutangazwa.

Mwisho

Total Views: 118 ,