usalama wameimarishwa katika Viwanja vya ndege

Usalama umeimarishwa vilivyo katika viwanja vikubwa vya ndege kufuatia ripoti za kijasusi kwamba magaidi wa Alsha baab wanapanga kutekeleza mashambulizi nchini.

Kulingana na taarifa hizo tayari magaidi 11 wa kujitolea mhanga kutoka kwa kundi hilo wamepewa mafunzo kutekeleza shambulizi hilo.

Aidha kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mamlaka ya usalama wa viwanja vya ndege ,mashambulizi hayo yaliyopangwa kutekelezwa mwishoni mwa mwezi huu na ujao yataelenga safari za ndege za humu nchini.

Total Views: 338 ,