Usalama pwani uko imara asema Marwa.

MARWA COASTIdara ya usalama imeweka mpango wa kuimarisha usalama katika kaunti zote 6 katika eneo la Pwani ili kukabiliana na tishio lolote la utovu wa usalama, wakati wa msimu wa sherehe za pasaka.

Mratibu wa eneo la Pwani Nelson Marwa amesema kuwa hatua hiyo imechukuliwa kufuatia shambulio la kigaidi jijini Brussels Ubelgiji hapo jana lililopelekea vifo vya watu wapatao 30 na kujeruhiwa wengine wengi.

Amewataka wakaazi kutoa taarifa kwa idara ya usalama wanapoona jambo lolote la kutia shaka.

Mwisho

Total Views: 418 ,