UJENZI WA BARABARA MSAMBWENI

Wakaazi wa eneo la Tukutane, eneo bunge la Msambweni kaunti ya Kwale wanapinga vikali hatua ya serikali ya kaunti hiyo ya kutaka jumla ya nyumba 15 kuvunjwa ili kutoa nafasi ya ujenzi wa barabara.

Wakaazi hao wanasema kwamba ujenzi wa barabara hiyo sio halali wakisema kuwa haiko katika ramani ya barabara ambazo zinafaa kufanyiwa ukarabati hivyo kuathiri pakubwa wakaazi wanaoishi katika sehemu hiyo.

picha hisani

Total Views: 29 ,