Uhuru atoa wito kwa Mataifa ya Afrika kuongeza Majeshi nchini Somalia

Rais Uhuru Kenyatta ametoa wito  kwa mataifa ya Afrika kuongeza wanajeshi nchini Somalia ili kuyapa nguvu zaidi majeshi ya KDF katika kukabiliana na mashambulizi ya wanamgambo wa Alshabaab.

Kiongozi huyo wa taifa anasema majeshi ya KDF yamekuwa katika hatari ya kushambuliwa kutokana na kutotumwa kwa  vikosi zaidi vya kulinda amani chini ya AMISOM nchini humo hasa katika eneo la Gedo ambalo hutumiwa  sana na kundi la Alshabaab kuwashambulia wanajeshi wa KDF.

Kwa sasa mataifa ya Kenya,Uganda,Djibout na Ethiopia yanawanajeshi wake wanaohudumu nchini Somalia chini ya AMISOM.

Kenya ilipata pigo zaidi baada ya wanajeshi wake kushambuliwa na kundi hilo la kigaidi katika kambi ya El Ade kusini mwa taifa la Somalia mwezi januari mwaka huu ambapo idadi isiyojulikana na wanajeshi hao waliuwawa.

Total Views: 546 ,