UHIFADHI WA MISITU KWALE

Idara ya uhifadhi wa misitu kwa ushirikiano na serikali kuu imeanzisha mradi wa upanzi wa miti ya mikoko katika bahari ya Vanga, na vijiji vitano katika eneo hilo kama njia mojawapo ya kuafika ajenda nne za serikali ya  kukuza uchumi wa bahari.

Akiongea na wanahabari eneo la Vanga wakati wa uzinduzi wa mradi huo Waziri wa maswala ya mazingira Keriako Tobiko amesema kuwa lengo kuu la uzinduzi huo ni kuhakikisha kuwa utunzaji wa bahari unaendelezwa Kwa njia inayostahili.

Aidha amesema kuwa mikoko imekuwa ikiharibiwa kiholela huku wakaazi wakikosa kufahamu thamani yake hali iliyoleta msukumo zaidi wa kuanzisha zoezi hilo.

Picha hisani

Total Views: 17 ,