Uajiri wa madaktari kutoka Tanzania kusubiri zaidi

Mahakama ya kushughulikia maswala ya leba nchini imeongeza mda wa kutekelezwa kwa agizo la kusitisha mpango wa kuajiriwa kwa madaktari wa kigeni hadi kesi iliyowasilishwa na wakenya wawili kupinga mpango huo itakaposikizwa na kuamuliwa.

Jaji wa mahakama hiyo Nelson Abuodha amepeana mda wa siku saba zaidi kwa pande zote mbili katika kesi hiyo kuwasilisha maelezo muhimu kuhusu kesi hiyo kabla ya kupeana muongozo kuhusu swala hilo terehe tano mwezi juni mwaka huu.

Kwenye kesi hiyo wakenya wawili madaktari ambao hawajaajiriwa wanahoji hekima ya baraza la magavana,waziri wa afya,tume ya huduma kwa umma,waziri wa maswala ya ndaniĀ  na muungano wa madaktari KMPDU dhidi ya kuajiriwa kwa madaktari wa kigeni.

Mwisho

Total Views: 305 ,